huduma zetu
HUDUMA MBALI MBALI ZINAZOPATIKANA MWENGE SDA
Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.

Huduma ya uinjilisti
Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.

Huduma ya Ubatizo
Yesu akajibu, Amini, amini nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na roho hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili na kilichozaliwa kwa roho ni roho

Huduma ya Maombi
Nitakupa funguo za ufalme wa mbinguni; kila utakachofunga duniani, kitafungwa pia mbinguni; kila utakachofungua duniani, kitafunguliwa pia mbinguni

Huduma za ibada
Bwana ni mwema wana na binti za Mungu. Karibuni sana katika kanisa letu tumsifu na kumtukuza Mungu aliye hai, kwa maana imeandikwa:-"Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao."

Huduma za ndoa na familia
Kwa Mkristo ahadi ya ndoa ni kwa Mungu na pia kwa mwenzi, na inapaswa kuingizwa tu kati ya mwanamume na mwanamke ambao wana imani moja. Upendo wa pande zote, heshima, heshima, na wajibu ni kiini cha uhusiano huu, ambao unapaswa kuakisi upendo, utakatifu, ukaribu, na kudumu kwa uhusiano kati ya Kristo na kanisa lake.

Huduma za uwakili
“Sisi tu Mawakili wa Mungu tuliokabidhiwa na yeye wakati, fursa, uwezo na mali na mibaraka ya dunia na rasimali zake. Tunawajibika kwake kwa matumizi yake sahihi. Tunakiri umilikaji wa Mungu kwa huduma ya uaminifu kwake na wanadamu wenzetu, na kwa kurudisha zaka na kutoa sadaka kwa ajili yake na kwa utegemezaji na ukuaji wa Kanisa lake. Uwakili ni fursa iliyotolewa kwetu na Mungu kwa ajili ya malezi katika upendo na ushindi dhidi yao choyo na tamaa. Wakili hufurahia mibaraka inayowajia wengine kama matokeo ya uaminifu wake” (Kanuni ya Kanisa toleo la 17 sura 3-12).
Kwanini huduma Mwenge SDA
Bwana akasema, Ni nani, basi, aliye wakili mwaminifu, mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya utumishi wake wote, awape watu posho kwa wakati wake? Nasi tunajibu tukisema:-
1 Wakoritho : Mlango 4
1 Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu. kupitia sisi utanufaika na mengi kama:-
- taaluma za kiroho: Tutajifunza na kufahamu maandiko.
- ushauri nasaha: misaada katika masuala mbali mbali.
- kutiana mioyo: Ibada na mikutano mbali mbali inafanyika kanisani
Utapata nini ukihudumiwa?
Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake? Ama mtu atoe nini badala ya nafsi yake?
- Amin, amin, nawaambia, Yeye aaminiye yuna uzima wa milele.
- kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya.