Juma la maombi

Maranatha watu wa Mungu. Karibuni katika sabato ya tarehe 02 / 04 / 2022 ambayo ni sabato ya kuanza juma la maombi. Washiriki wote tunawakumbusha kuwa katika sabato hii tutaanza juma letu la maombi. Tunawakaribisha sana wageni popote ulimwenguni ili Bwana atubariki pamoja, kwa wageni walioko Dar es Salaam tutafurahi mkijumuika nasi katika kanisa letu lililopo mita 100 kutoka barabara ya Ali Hassan Mwinyi mkabala na kituo cha afya cha Mwenge, tunawakaribisha sana maana katika siku hii tutakuwa na programu nyingi nzuri kama meza ya bwana na sadaka ya majengo ili tumjengee Mungu wetu. Kwa wageni waliombali tunapenda mjumuike nasi mubashara kupitia mitandao yetu ya kijamii yaani Instagram, Facebook au Youtube ili tubalikiwe pamoja, pia mnaweza kushiriki nasi katika uchangiaji wa ujenzi wa jengo letu kupitia bank na Bwana atawabariki. Mungu awabariki wote na karibuni sana.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *