Events

April 23 / 2022 / 09:00 AM

Kanisa la waadventista wa sabato Mwenge linapenda kukukaribisha / kuwakaribisha, KARIBUNI SANA.

Leo ni sabato maalum kwaajil ya watu wenye mahitaji maalum. Pia mchana kutakuwa na mada maalum kwa vijana wakubwa ( 22 – 35+ ) juu ya changamoto za mahusiona kwenye jengo jipya gorofa ya kwanza. Wawezeshaji ni Awadia Ogillo, Anna Matinde na Jacobo Kihila. Vijana mnahimizwa kuwahi.

Mkutano mkuu wa kanisa utafanyika tarehe 01 / 05 / 2022 kuanzia saa 03:00 asubuhi. Wote wenye ushirika Mwenge mnaohimizwa kuhudhuria.

Kesho tarehe 24 / 04 / kutakuwa na PICNIC ya watoto wetu ni WILD KUNDUCH Kiingilio, chakula na usafiri ni Tsh 25,000. Wazazi mnaombwa muwaandikishe watoto kwa kiongozi wa watoto Eunice Mshuda. Mwisho wa kutoa kingilio ni leo jioni. Muda kuondoka ni saa 2:30 asubuhi. 

April 30 / 2022 / 9:00 AM

Kanisa la waadventista wa sabato Mwenge linapenda kukukaribisha / kuwakaribisha, KARIBUNI SANA.

Sabato ijayo 30 / 04 / 2022 tutakuwa na ubatizo hapa kanisani. Wote wanao kusudia kubatizwa waonane na uongozi wa kanisa.

 Sabato ya tarehe 30 / 04 / 2022 tutatoa sadaka ya uinjilisti. Wote tunahimizwa kuandaa sadaka zetu za uinjilisti.

Efoti ya redio iliyoanza trehe 03 /04 / 2022 inaendelea hadi tarehe 30 / 04 / 2022 kila siku saa 5:15 asbuhi hadi saa 6:00 mchana isipokuwa siku ya jumamosi. Mhudumu ni mchungaji Elitabu Kajiru. Wote mnakaribishwa kuifatilia, kuwahimiza ndugu, jamaa na marafiki kuifatilia kupitia FM 105.3.

May 08 / 2022 / 8:00 AM

Kanisa la waadventista wa sabato Mwenge linapenda kukukaribisha / kuwakaribisha, KARIBUNI SANA.

Kutakuwa na semina Maalum ya Idara ya huduma za watoto kuanzia tarehe 08 / 05 / 2022 hadi tarehe 10 / 05 / 2022 huko Dodoma kwenye chuo chetu cha kanisa. Wahusika ni viongozi wa idara ya huduma ya watoto, walimu wote wanaofundisha watoto na wazee wa idara. Kiingilio ni sh. 20,000=/, Bima sh. 2,000/=, Malazi sh. 5,000 /= na chakula sh. 6,000/= kwa siku kutegemea na aina ya chakula. Fedha  itumwe kwenye Account ya CRDB Bank, SDA Church ECT No. 0150319513600. Mwisho wa kutuma ni tarehe 15 / 04 / 2022.

Tuendelee kutoa sadaka zetu za majengo ya maandalizi ya kumwaga zege la Mezanine itakayojengwa kufikia mwezi Mei. Wote waliotoa ahadi mnakumbushwa kuzikamilisha na pia tuendelee kuleta vifaa.

Makambi ya mtaa wa Mwenge yatafanyika tarehe 10 / 04 / hadi 16 / 04 / 2022. Bajeti ya matumizi ni Tsh 44.8 M. Viwango elekezi vya sadaka ni :-

  • wafanyakazi / wafanyabiashara / wana ndoa 250,000/= ( 50,000 kila mwezi )
  • wasio na ndoa 150,000/= ( 30, 000 kila mwezi )
  • wanachuo 25,000/= ( 5,000 kila mwezi ) 
  • watoto 10,000/= ( 2,000 kila mwezi ). Mpango wa utoaji umeanza mwezi Februari na kuisha June.