Hapo mwaka 1985 ilibainika kwamba kundi la Mwenge limekuwa na hadhi ya kutengwa na kufanywa kanisa japo halikuwa na jengo la kusalia linalofaa. Lilikuwa limetimiza taratibu zilizotakiwa na pia lilikuwa na watu wanaofaa kuongoza kanisa linalojitegemea kufuatana na kanuni ya Kanisa. Soma kanuni ya kanisa uk.163. Zaidi ya hapo kundi hili lilikuwa na vifaa vya meza ya Bwana  vilivyohitajika na kabatikubwa la kuwekea vifaa hivyo. Baadhi ya washiriki waanzilishi ni K.B. Elineema, Jotham Lukwaro, Daudi Nyaruhucha, Naghenjwa Lukwaro, John Nyika, Peninah Matiko, Loveness Nyika, Nehemiah Matiko, Tezra Kerenge, Anna Nyaruhucha, Josphat Mchunde, Perida Kisama, Dorah Machunde na Milka Muso.

Baraza la kwanza la Kanisa la Mwenge lilikuwa na wajumbe wafuatao: Zakayo Kerenge (Mwenyekiti), K.B. Elineema, Amos Mwakalinga, Jotham Lukwaro, Daudi Kanakoko, A.O. Mwambogela, O.S. Mtani, Daudi Nyaruhucha, Nehemiah Matiko, Beatrice Mwakalinga, Onica Mwambogela, Zephania Rhobi na Fanuel Gichengwe.

Watu waliohudumu kwenye Kanisa la Mwenge kwa vipindi mbalimbali kama Wazee wa kwanza ni Zakayo Kerenge, K.B. Elineema, John Muso, Daudi Kanakoko, Jotham Lukwaro, Msafiri Jackson, Finehas Chogero, Sifael Hango na Rajab Kiravu.

Hapo Januari 25, 1995 Kanisa la Mwenge lilibahatika kutembelewa na viongozi wa juu wa kazi ya Mungu. Viongozi hao ni Mchungaji Dr. Robert Folkenberg, aliyekuwa Kiongozi Mkuu Duniani wa kanisa la Waadventista Wasabato na Dr. Mchungaji L.D. Raelly aliyekuwa Kiongozi wa Divisheni ya Mashariki ya Afrika. Mchungaji Dr. Folkenberg aliingia ndani ya Kanisa na kumwomba Mungu alibariki Kanisa na washiriki wote wanapojitayarisha kwa kurudi kwa Bwana wetu Yesu.