Pamoja na kazi za jengo la kanisa la mwenge, waumini wake wamefanya kazi ya utume ili kujiandaa na kuwaandaa wengine kwa kumaliza kazi ya Mungu na kujitayarisha kwa uzima wa milele. Kila mwaka kanisa la Mwenge limeshiriki kwenye mahubiri ya nyumba kwa nyumba na pia yale ya hadhara. Kila mkutano wa mahubiri hayo ya hadhara umefanyika kwa muda wa wiki tatu mfululizo. Tangu mwaka 1985 mahubiri ya hadhara zaidi ya 28 yamefanyika na kanisa la mwenge nakupata waumini wapya zaidi ya 900 kutokana na kazi hiyo. Miongoni mwa hao zaidi ya 600 walibatizwa na kujiunga na Kanisa la Waadventista wa Sabato. Mahubiri hayo yamefanyika kuanzia maeneo ya Mwenge hadi Bagamoyo na yameligharimu kanisa la mwenge zaidi ya shilingi milionni 24.6. Tangu mwaka 2000  kanisa la mwenge limekuwalikifanya mahubiri yahadhara yasiyopungua manne kila mwaka. Pia shughuli mbalimbali za kufundisha Biblia kwa njia ya posta zimefanyika na wahitimu wamepewavyeti vyao.

Shughuli zingine zilizofanywa na Kanisa la mwenge ni kuwaendea wagonjwa, walemavu, yatima, mahospitalini, magerezani na wenye misiba ili kuwafariji na kuwahudumia kiroho na pia kwa hali na mali.

Tangu mwaka 1985 hadi leo Kanisa la Mwenge limeanzisha makundi tisa na kuyalea. Kati ya hayo sita yameshapewa hadhi ya kuwa makanisa. Hayo ni Tegeta, Lugalo, Ushindi, Bagamoyo, Bunju na Kerege. Makundi yake ya Zinga, Mabwepande na Kimele yanaendelea kulelewa. Mwenge imejenga majengo ya kudumu ya kuabudia kwenye makundi hayo. Zaidi ya hapo kanisa la mwenge limeajiri wainjilisti walei wanaohudumia Makundi hayo na pia lina Mwinjilisti mmoja aliyebobea kwenye elimu ya Kurani na masuala ya Kiislamu.

Wachungaji ambao wamehudumia Kanisa la Mwenge tangu likiwa kundi hadi leo ni John Moses, Elias Timasi, E.Hume, E.Munguruta, E.Mganga, Joram Japheth, Bright Nyerembe, Eliezer A.Sabuni, Stephen Ngussa, Michael Twakaniki na Pr. William Mshana.

Kuwekwa Wakfu
Jengo la Kanisa la Mwenge lilianza kujengwa mwaka 1987 na liliwekwa wakfu tarehe 22 December, 2002 na Pr. Dr. Herry Mhando mhubiri wa kimataifa wa waadventista wasabato.