Waumini wa kanisa la Waadventistawasabato Mwenge, hawana lugha ya kutumia au gharama ya kumrudishia Mungu mumba wa mbingu na nchi kwa kukubali kuruhusu jengo hili lilivyo leo, liweze kuwa miongoni mwa majengo mengi yanayozunguka Jiji hili la dar es salaam liitwe Nyumba yake ya sala kwa mataifa yote.

Kanisa la Wasabto Mwenge ni miongoni mwa makanisa mengi ya kisabato ambayo yamefunguliwa kwenye Jiji la Dar es salaam. Kanisa la Mwenge liko kilometa 15 hivi toka katikati ya jiji kando kando ya barabara iendayo Bagamoyo kwenye eneo la Mwenge. Katika kijiji hiki cha Mwenge ambapo kanisa hili lipo kuna makanisa ya Kikatoliki kilutheri, Kibaptista ,Assemblies of God , Anglikana na pia Msikiti wa Waislamu kwenye eneo hili.