Archive report here

Pamoja na kazi za jengo la kanisa la mwenge, waumini wake wamefanya kazi ya utume ili kujiandaa na kuwaandaa wengine kwa kumaliza kazi ya Mungu na kujitayarisha kwa uzima wa milele. Kila mwaka kanisa la Mwenge limeshiriki kwenye mahubiri ya nyumba kwa nyumba na pia yale ya hadhara. Kila mkutano wa mahubiri hayo ya hadhara umefanyika kwa muda wa wiki tatu mfululizo. Tangu mwaka 1985 mahubiri ya hadhara zaidi ya 28 yamefanyika na kanisa la mwenge nakupata waumini wapya zaidi ya 900 kutokana na kazi hiyo. Miongoni mwa hao zaidi ya 600 walibatizwa na kujiunga na Kanisa la Waadventista wa Sabato. Mahubiri hayo yamefanyika kuanzia maeneo ya Mwenge hadi Bagamoyo na yameligharimu kanisa la mwenge zaidi ya shilingi milionni 24.6. Tangu mwaka 2000  kanisa la mwenge limekuwalikifanya mahubiri yahadhara yasiyopungua manne kila mwaka. Pia shughuli mbalimbali za kufundisha Biblia kwa njia ya posta zimefanyika na wahitimu wamepewavyeti vyao.

Shughuli zingine zilizofanywa na Kanisa la mwenge ni kuwaendea wagonjwa, walemavu, yatima, mahospitalini, magerezani na wenye misiba ili kuwafariji na kuwahudumia kiroho na pia kwa hali na mali.

Tangu mwaka 1985 hadi leo Kanisa la Mwenge limeanzisha makundi tisa na kuyalea. Kati ya hayo sita yameshapewa hadhi ya kuwa makanisa. Hayo ni Tegeta, Lugalo, Ushindi, Bagamoyo, Bunju na Kerege. Makundi yake ya Zinga, Mabwepande na Kimele yanaendelea kulelewa. Mwenge imejenga majengo ya kudumu ya kuabudia kwenye makundi hayo. Zaidi ya hapo kanisa la mwenge limeajiri wainjilisti walei wanaohudumia Makundi hayo na pia lina Mwinjilisti mmoja aliyebobea kwenye elimu ya Kurani na masuala ya Kiislamu.

Wachungaji ambao wamehudumia Kanisa la Mwenge tangu likiwa kundi hadi leo ni John Moses, Elias Timasi, E.Hume, E.Munguruta, E.Mganga, Joram Japheth, Bright Nyerembe, Eliezer A.Sabuni, Stephen Ngussa, Michael Twakaniki na Pr. William Mshana.

Kuwekwa Wakfu
Jengo la Kanisa la Mwenge lilianza kujengwa mwaka 1987 na liliwekwa wakfu tarehe 22 December, 2002 na Pr. Dr. Herry Mhando mhubiri wa kimataifa wa waadventista wasabato.

Mchoraji wa ramani za jengo alikuwa Ndugu Daudi Kanakoko lakini upimaji wa jengo ulifanywa na mhandisi Peter Mkwizu akishirikiana na Isaac Nyagabona. Baada ya hapo Isaac Nyagabona aliendelea kufanya kazi hiyo na wahandisi wengine waliofuatia kama Sylvester Mayunga na Mkohi Kichogo walisaidia sana. Waumini wote walipeana majukumu ili kuhakikisha kazi inafanyika. Baadhi ya taratibu zilizotumiwa kupata michango ni pamoja na:

 1. Kuandika barua kwa makanisa ya Dar es salaam kuomba michango
 2. Mpango wa kuchangisha uliandaliwa na Idara ya Majengo.
 3. Matembezi ya hisani yalifanyika toka Kanisa la Magomeni kupitia Kinondoni hadi Mwenge. Matembezi haya ni yakilomita 10.
 4. Mh A.L. Mrema, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani wakati huo alisaidia kuhamasisha watu kwenye mkutano maalum kuchangia ujenzi wa jengo la Kanisa Mwenge.
 5. Balozi Charles Nyirabu ambaye kwa wakati huo alikuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania alitoa mchango napia kukubali ombi la kuwa Mdhamini wa jengo hilo.
 6. Barua mbalimbali ziliandikwa viwandani kuomba michango.
 7. Maombi mengi yalifanyika kuombea kazi ya ujenzi wa kanisa hilo.

Jengo lilipoanza lilipangwa liwe na ghorofa (balconies) tatu. Ilipofika mwaka 1990 mambo yote ya msingi yalikuwa yamekamilika, nguzo hadi msingi wa kati (ring beams) Hata hivyo, baadaye ilionekana kwamba itachukua muda mrefu kukamilisha kazi hiyo kama tusipopata wafadhili. Kutokana na hayo, kikao killikaa na kujadili kwakirefu na uamuzi ulifikiwa kwamba michoro ibadilishwe na balconies ziachwe.

Hapo mwaka 1985 ilibainika kwamba kundi la Mwenge limekuwa na hadhi ya kutengwa na kufanywa kanisa japo halikuwa na jengo la kusalia linalofaa. Lilikuwa limetimiza taratibu zilizotakiwa na pia lilikuwa na watu wanaofaa kuongoza kanisa linalojitegemea kufuatana na kanuni ya Kanisa. Soma kanuni ya kanisa uk.163. Zaidi ya hapo kundi hili lilikuwa na vifaa vya meza ya Bwana  vilivyohitajika na kabatikubwa la kuwekea vifaa hivyo. Baadhi ya washiriki waanzilishi ni K.B. Elineema, Jotham Lukwaro, Daudi Nyaruhucha, Naghenjwa Lukwaro, John Nyika, Peninah Matiko, Loveness Nyika, Nehemiah Matiko, Tezra Kerenge, Anna Nyaruhucha, Josphat Mchunde, Perida Kisama, Dorah Machunde na Milka Muso.

Baraza la kwanza la Kanisa la Mwenge lilikuwa na wajumbe wafuatao: Zakayo Kerenge (Mwenyekiti), K.B. Elineema, Amos Mwakalinga, Jotham Lukwaro, Daudi Kanakoko, A.O. Mwambogela, O.S. Mtani, Daudi Nyaruhucha, Nehemiah Matiko, Beatrice Mwakalinga, Onica Mwambogela, Zephania Rhobi na Fanuel Gichengwe.

Watu waliohudumu kwenye Kanisa la Mwenge kwa vipindi mbalimbali kama Wazee wa kwanza ni Zakayo Kerenge, K.B. Elineema, John Muso, Daudi Kanakoko, Jotham Lukwaro, Msafiri Jackson, Finehas Chogero, Sifael Hango na Rajab Kiravu.

Hapo Januari 25, 1995 Kanisa la Mwenge lilibahatika kutembelewa na viongozi wa juu wa kazi ya Mungu. Viongozi hao ni Mchungaji Dr. Robert Folkenberg, aliyekuwa Kiongozi Mkuu Duniani wa kanisa la Waadventista Wasabato na Dr. Mchungaji L.D. Raelly aliyekuwa Kiongozi wa Divisheni ya Mashariki ya Afrika. Mchungaji Dr. Folkenberg aliingia ndani ya Kanisa na kumwomba Mungu alibariki Kanisa na washiriki wote wanapojitayarisha kwa kurudi kwa Bwana wetu Yesu.